MO DEWJI AFANYA MAKUBWA SIMBA SC... aanzisha mchakato wa kuirejesha timu kwenye makali yake

BILIONEA wa Simba Sc, Mohammed Dewji imeanzisha mchakato wa kuirejesha timu hiyo katika makali yake, imefanikiwa.

Habari ambazo zimepatikana zinasema kwamba Mohamed ambaye ameshaomba kumiliki hisa za Simba ya asilimia 51, ameikopesha Simba kiasi cha shil. bil 1, ili iweze kujiendesha.

Dewji ambaye ndie mmiliki wa kampuni ya Mo, amedaiwa kutoa kiasi hicho cha fedha ili Simba ifike kwenye mchakato ambao wameuanzisha kisha azikate kwenye mpango huo.

“Ni kweli kwamba Simba kwa sasa ikokwenye wakati mzuri sana unajua kwamba kili kitu ikiwemo mishahara Mo anatusaidia lakini sikwamba fedha hizo anatoa bure. Hatutaki uwezekanaji huu uwe bure maana Simba inatazama mbali,” mmoja wa wadau wakubwa katika Simba amesema.
Dewji imedaiwa ndie aliyewazuia baadhi ya wachezaji wa Simba wanaotaka kuondoka wakati mikataba yao ikimalizika kimaendeleo kwamba kwa sasa hapa Tanzania ni Simba pekee ndiko kwenye uhakika wa maisha bora.

 Dewji amesikia kwamba kuna wachezaji wanataka kuondoka wakati huu mikataba yao ikikaribia wasaini mikataba mipya haraka na mambo mengine wamwachie yeye," alisema mdau huyo.

“Anachofanya Mo kwa sasa anaitazama Simba anaona kuna wachezaji sio rahisi kuwaachia kwabababu mchakato wa kuichukua Simba unakwenda vizuri hawezi kukubali kuwapoteza wachezaji ambao wamekuwa wakifanya vizuri katika Ligi Kuu na mashindano mengine.”

Inaelezwa kwamba mfanyabiashara huyo amewataka wachezaji kupambana kuhakikisha kuwa Simba inachukua moja ya nafasi za uwakilishi wa michezo ya kimataifa lakini amewahakikishia kwamba mipango ya kuileta Juventus ya Italia kuungana na Simba katika uendeshaji mpira iko mbioni.

No comments