MONACO SIO WATU WA MCHEZO MCHEZO, WAILAZA BORUSSIA DORTMUND 3-2 ...Kylian Mbappe tishio


Monaco ya Ufaransa imeendelea kuonyesha kuwa sio timu ya kubeza baada ya kuinyuka Borussia Dortmund ya Ujerumani 3-2 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Champions League.

Mshambuliaji kinda anayewaniwa na vigogo kadhaa barani Ulaya, ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo huku akitupia wavuni mabao mawili.

Wakiwa ugenini, Monaco walikuwa wa kwanza kupata bao la kwanza mfungaji akiwa ni Kylian Mbappe dakika ya 19 kabla ya Sven Bender hajajifunga dakika ya 35 na kufanya wageni waende mapumziko wakiwa mbele 2-0.

Ousmane Dembele akaifungia Borussia Dortmund bao la kwanza dakika ya 57 lakini Kylian Mbappe akawa mwiba tena kwa kuifungia Monaco goli la tatu 79 huku nyota wa zamani wa Manchester United Shinji Kagawa akiwapa wenyeji bao la pili dakika ya 84.

No comments