MONACO WASIKIE HIVYO HIVYO, BORUSSIA DORTMUND YAKALISHWA 3-1 …Mbappe, Falcao moto chini


Monaco imeifumua Borussia Dortmund 3-1 na kutinga nusu fainali ya Champions League kwa jumla ya mabao 6-3 kufuatia ushindi wa 3-2 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ujerumani.

Mshambuliaji kinda Kylian Mbappe aliyeisumbua sana ngome ya Borussia alifunga bao la kwanza dakika ya tatu huku Radamel Falcao akitupia la pili dakika ya 17.

Kiungo Marco Reus akaifungia bao pekee Borussia dakika ya 48 kabla Valere Germain hajaipa Monaco goli la tatu dakika ya 81.

No comments