MOSE IYOBO AANZISHA DARASA LA KUFUNDISHA MUZIKI DAR

DANSA anayetoka kwenye kundi la la Wasafi Moses Iyobo amepanga kuanzisha darasa la muziki nchini.

Iyobo ambaye ni dansa mkuu wa Diamond, alizungumza na chombo kimoja cha habari na kuweka wazi juu ya mpango huo ambao upo mbioni kuanza.

“Najua mtaani kuna vipaji vingi lakini vimekosa matunzo, mpango wangu ni kuanzisha darasa maalum kwa ajili ya masuala ya dansa ili kuikuza tasnia ya burudani nchini,” alisema staa huyo.

"Mimi ni dansa siku nyingi, najua changamoto zinazowakumba watu wenye fani kama yangu huko mitaani ndiyo maana ninaona ni bora kuanzisha darasa litakaloweza kuwainua kisanii.”


"Hata mimi wapo watu walionisaidia mpaka kufikia mafanikio njiinayo hivyo naona ni vema na mimi nikatoa sapoti kwa wsatu waliocjhini na watatafuta namna ya kutoa,” alimaliza Iyobo.

No comments