MOSE IYOBO ASEMA HANA MPANGO WA KUJIINGIZA KWENYE UIMBAJI

MNENGUAJI wa Diamond Platnumz, Mose Iyobo amesema kwamba hana mpango wa kuimba na kwamba yeye ataendelea na kazi anayoifanya hivi sasa ya unenguaji.

Akiongea na Saluti5, Iyobo amesema hana mpango huo kwa kuwa kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe, hivyo kwa upande wake hataweza kufanya hivyo na ni bora aendelee na kazi yake anayoifanya sasa.

“Unajua, kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe, sasa kwa upande wangu sitaweza. Bora nibaki hukuhuku ndio kunanifaa zaidi,” amesema Iyobo.


Ameongeza kuwa labda kitu ambacho atakiongeza kukifanya ni kuwa mwalimu na kuwafundisha vijana wengine jinsi ya kucheza.

No comments