Habari

MOURINHO AMTAKA CLAUDE MAKELELE MPYA MANCHESTER UNITED

on

Jose Mourinho ameiambia bodi ya Manchester United kuhakikisha inasajili kiungo halisi mkabaji aina ya Claude Makelele baada ya kukiri kushindwa kupigania taji msimu huu.
Kocha huyo ameyasema hayo baada ya kushindwa kumsajili N’Golo Kante aliyetua Chelsea kiangazi kilichopita.
Mourinho alimuona Kante kama mtu sahihi wa kucheza nyuma ya Pobga mara tu aliposaini mkataba wa kuikochi Manchester United lakini juhudi zake zikagonga mwamba baada ya nyota huyo wa zamani wa Leicester City na timu ya taifa ya Ufaransa kuweka wazi kuwa anakwenda Stamford Bridge.
Mourinho ameanza kupiga hesabu za kuijenga upya United kwa msimu ujao na hakuna ubishi  kuwa atasajili kiungo baada ya kuwaondoa   Morgan Schneiderlin na Bastian Schweinsteiger.
Claude Makelele alikuwa nguzo ya Mourinho katika msimu wake wa kwanza wa kuikochi Chelsea na kutwaa taji la Premier League 2006–07 kwa rekodi ya pointi 95.
Aliporejea kwa mara ya pili Chelsea, Mourinho akafanikiwa tena kuipa taji Chelsea kwa kumrejesha kiungo mkabaji Nemanja Matic na kuzoa ubingwa wa 2014/15.
Kwa kumpata  aina ya mtu kama Makelele au Kante, Mourinho anaamini Pobga atakuwa huru zaidi na kudhihirisha uwezo wake uwanjani. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *