MOURINHO AMTAKA DE GEA ASAHAU KUHUSU REAL MADRID


Jose Mourinho amemwambia David de Gea aweke kando kabisa mawazo ya  kuondoka Manchester United na kujiunga Real Madrid.

Kocha huyo wa United amemwambia De Gea muda sahihi ya kuwa na fikra hizo ni baada ya msimu kukamilika na kamwe si kabla ya hapo.

Hatma ya De Gea ndani ya Old Trafford imeingia tena mashakani baada ya mlinda mlango huyo kupigwa benchi kwenye mchezo dhidi ya Sunderland Jumapili iliyopita. 

Sababu rasmi zilizotajwa kwa De Gea kuachwa kwenye mchezo huo ni maumivu ya paja, lakini inaeleweka kuwa Mourinho alikosoa kwa siri kiwango cha kipa huyo hususan kwenye michezo dhidi ya West Brom na Everton. 

No comments