Habari

MOURINHO ASEMA ATAINGIA VITANI KWA WACHEZAJI ALIONAO …aweka kando visingizio vya majeruhi

on

Leo usiku Manchester United inaingia vitani na Manchester City katika mchezo muhimu wa Premier League ambao unaweza kutoa picha ya mwelekeo wa ‘top four’.
Hata hivyo United itacheza mchezo huo huku ikiwa na mapengo kadhaa ya wachezaji wake muhimu wakiwemo Paul Pobga, Zlatan Ibrahimovic, Chris Smalling, Phil Jones, Marcos Rojo na Juan Mata ambao wote ni majeruhi.
Kocha wa United Jose Mourinho amekiri kuwa timu yake ipo kwenye janga kubwa la majeruhi lakini akasema hilo sio tatizo na anawaamini vijana wake.
“Tutakwenda na wachezaji tulio nao, tutapambana kwa kile tulichonacho. Ninawaamini vijana wangu na wapo tayari”, alisema Mourinho.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *