Habari

MOURINHO ASEMA HAOFII KUKOROMEA WACHEZAJI WAKE

on

Kocha wa Manchester United  Jose Mourinho amesema hajali kuwa kitendo chake cha kukosoa na kuwakoromea wachezaji wake wanaovurunda uwanjani, kunaweza kuwa ni sawa na kucheza ‘pata potea’.
Mourinho amesema  kwake yeye anaona ni jambo linalojihitaji kutumia akili ya kawaida. Kama mchezaji hatimizi wajibu wake kwa asilimia 100, hawezi kumfumbia macho.
Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wakiwemo  Luke Shaw na Anthony Martial wamekumbana na joto la Mourinho kwa kukosolewa hadharani. 
Alipoulizwa iwapo haoni kuwa tabia hiyo inaweza kutibua amani kwa wachezaji wake, Mourinho akaiambia Sky Sports “Sijali. Wala hata sifikirii hilo jambo. Sio suala la mbinu za kisaikolojia. 
“Najaribu kuwa vile nilivyo. Najitahidi kuwa muwazi na muungwana na sifikirii kuhusu matokeo mbadala.
“Ukijituma na kutoa matokeo chanya nitakupongeza kwa hilo. Ukifanya kinyume chake nitakukosa. Ni jambo la kawaida.”

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *