MOURINHO ASEMA MAN CITY HAIZULIKI TOP FOUR …adai vita imebaki kwa United, Liverpool na Arsenal


Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema anadhani Manchester City watamaliza katika ‘top four’ ya Premier League.

Kutokana na hali hiyo, Mourinho anadai nafasi iliyobaki ni moja na inagombewa na timu tatu – Manchester United, Liverpool na Arsenal.

Akiongea katika mkutano wa waandishi wa habari baada ya mechi ya jana usiku kati Manchester United na Manchester City Mourinho alisema: “Nadhani City watamaliza ‘top four’.

“Nikiangalia uchezaji wao na mechi walizobakiza, naona hawana kizuizi cha kutinga top four.

“Nafasi imebaki moja – ni kati yetu sisi, Arsenal au Liverpool. Ni hatua ngumu lakini tutapambana hadi mwisho”.

No comments