Habari

MOURINHO LAWAMANI KWA NAMNA ANAVYOWAPELEKESHA PHIL JONES NA CHRIS SMALLING

on

Inaaminika kuwa baadhi ya wachezaji nyota wa Manchester United wanakerwa na namna Jose Mourinho anavyowachukulia majeruhi  Chris Smalling and Phil Jones.
Mourinho mara mbili amewashutumu mabeki hao wawili na kusema kama wanajitoa kwa moyo wao wote kwaajili ya timu basi wanapaswa kucheza mchezo wa Alhamisi dhidi ya Manchester City.
Hapo kabla Mourinho alisema kwa mdomo wake mwenyewe kuwa Smalling atarejea uwanjani katikati ya mwezi Mei, lakini sasa baada ya Marcos Rojo kuumia, kocha huyo Mreno ameyameza maneno yake na kutaka huduma ya Smalling ambaye bado hajapona kisawasawa. 
Jones, aliyeonekana mazoezini Jumanne ndani ya Carrington anaelekea kupona na bado haijajulikana kama ataitikia wito wa Mourinho na kucheza Alhamisi. 
Eric Bailly anabakia kama beki pekee wa kati akitarajiwa kucheza na mchezaji kiraka Daley Blind. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *