MOURINHO MIKONONI MWA CELTA VIGO ...Jurgen Klopp aipa Man United ubingwa Europa League


Manchester United chini ya kocha Jose Murinho imepangiwa Celta Vigo ya Hispania kwenye nusu fainali ya  Europa League.

Vijana hao wa Jose Mourinho watacheza mchezo wa kwanza ugenini  Mei 4 kabla ya mchezo wa marudiano Old Trafford Mei 11.

Nusu fainali nyingine itakuwa kati ya   Ajax ya Holland dhidi ya Lyon ambapo mchezo wa kwanza utachezwa Amsterdam.

United  haijawahi kukutana na Celta Vigo katika michuano yoyote ile, lakini wanapewa na nafasi kubwa ya kusonga mbele dhidi ya timu hiyo iliyoko katikati ya msimamo wa La Liga.

Kabla ya mchezo wa marudiano wa robo fainali dhidi ya  Anderlecht Alhamisi usiku, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp aliipa nafasi kubwa Manchester United ya kutwaa taji la Europa League.

Klopp akasema haoni ni namna gani United itashindwa kufika fainali na kama watafika hatua hiyo huku wakiwa na wachezaji wote muhimu, basi miamba hiyo ya Old Trafford itatwaa ubingwa.

Manchester United inategemewa kuwa bila wachezaji wake watano muhimu ambao wote ni majeruhi Zlatan Ibrahimovic, Marcos Rojo, Juan Mata, Chris Smalling na Phil Jones.   

No comments