Habari

MOURINHO: TUJILAMU WENYEWE KWA KUSHINDWA KUZITUMIA NAFASI

on

Jose Mourinho amewashutumu washambuliaji wake kwa kuwa wazembe na kushindwa kuzitumia nafasi wakati   Manchester United ilipolazimishwa sare ya 1-1 na  Anderlecht Alhamisi usiku.

Henrikh Mkhitaryan aliitanguliza  United kwenye mchezo huo wa kwanza wa robo fainali ya  Europa League lakini vinara wa ligi ya Ubelgiji wakasawazisha ukingoni mwa mchezo kupitia kwa  Leander Dendoncker.
“Tunapaswa kumaliza mchezo mapema,” alisema Mourinho. “Tulipata nafasi nyingi, tulisatahili kufunga. Tumeshindwa kudumbukiza mipira wavuni.
“Tulikuwa na kila namna ya kushinda mchezo. Tunapaswa kujilaumu wenyewe kwasababu tulikuwa na mchezo mwepesi lakini tulishindwa kushambulia kwa jicho la ‘uuaji’.  Marcus Rashford, Jesse Lingard, Zlatan Ibrahimovic, Anthony Martial hawakuwa tishio.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *