MPIRA WA WAVU WAPATA KIKOSI CHA TIMU YA VIJANA YA TAIFA

CHAMA cha mpira wa wavu nchini kimesema kuwa kimefanikiwa kupata timu ya vijana itakayoandaliwa kwa ajili ya kushiriki katika mashindano ya kimataifa.

Timu hiyo imepatikana kupitia mashindano ya Klabu Bingwa ya Wavu Muungano yaliyoshirikisha klabu za Tanzania Bara na Zanzibar.

Akiongea na saluti5, katibu msaidizi wa Tava, Alfred Selengia alisema kuwa timu ya vijana imepatikana na itaandaliwa kwa kufundishwa na mtaalam kutoka Japan.

Alisema kuwa, Kamati ya ufundi imefanya kazi yake ya kuangalia vipaji vya wachezaji kupitia mashindano hayo.
Selengia alisema kuwa kikosi cha timu hiyo kitatangazwa baadae kwa ajili ya maandalizi.

“Kwa kweli tumeweza kufanikiwa kupata vijana katika mashindano yetu haya, hivyo tunaamini tutakuwa na timu itakayoanza kufundishwa na walimu wazawa kwa kumshirikisha pia Mjapan atakayekuja nchini,” alisema Selengia.


Sanjali na hilo, pia mashindano hayo yametoa fursa kwa ajili ya kuchagua timu ya wakubwa ambapo watajiandaa kwa ajili ya michezo ya kimataifa.

No comments