MR T TOUCH ATHIBITISHA KUMSAJILI YOUNG DEE TOUCHEZ SOUND RECORDS

PRODUZA wa muziki Mr. T Touch amethibitisha kumsajili Young Dee kwenye lebo yake ya “Touchez Sound Records” kwa miaka mitatu.

Mtayarishaji huyo wa muziki amekiambia kipindi cha E-News cha EATV kuwa yeye atakuwa anasimamia na kutengeneza beat za nyimbo zote za msanii huyo.

“Mimi nimeingia mkataba mrefu wa miaka mitatu na Young Dee, ataendelea kuwepo chini ya Touchez Sound Records na mimi ndie nitakayesimamia na kutengeneza beat za nyimbo zote.”

“Nia yangu ni kumfanya afanye vitu tofauti na alivyokuwa akifanya hapo awali kwa kuwa mimi ninamuona ni msanii wa kibiashara,” amesema Touch.

Young Dee alikuwa anasimamiwa kazi zake na MDB ya Max Rioba kabla ya kutangaza kuachana nae mapema mwanzoni mwa mwaka huu.

No comments