MSONDO NGOMA FAMILY DAY SASA KILA MWEZI KAMA KAWA... kupumzika mwezi Juni pekee mwaka huu

NYOMI walilolipata kwenye shoo yao ya “Msondo Ngoma Family Day” lililorindima Jumapili ya Pasaka ndani ya Bulyaga, Temeke, limewafanya Msondo Ngoma Music Band kutangaza kuendelea na utaratibu wao wa kila mwezi wa shoo hiyo.

Akiongea na saluti5, Kiongozi wa Msondo Ngoma, Juma Katundu amesema kuwa zaidi ya mashabiki 300 waliowapata kwenye shoo ya Jumapili ya Pasaka imewatia moyo kuendelea na utaratibu wao ambao kwa maelezo yao, waliusimamisha kwa muda kutokana na majukumu ya mwaka mpya.

“Tamasha la Msondo Ngoma Family Day sasa litaendelea kama kawaida na baada ya Jumapili ya Pasaka, mwishoni mwa mwezi Mei tutafanya linguine katika ukumbi tutakaoutaja baadae,” amesema Katundu.


Katundu amesema kuwa, watapumzika mwezi Juni pekee kupisha mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhani, lakini baada ya hapo utaratibu utaendelea kama kawaida.

No comments