MSUVA ASEMA KIPIGO WALICHOWAPA PRISONS NI SALAMU KWA TIMU NYINGINE ZILIZOBAKI

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Simon Msuva amesema kipigo cha mabao 3-0 walichokitoa kwa Prisons ni dalili mbaya kwa timu pinzani watakazokutana nazo katika kumalizia msimu baada ya safu yao ya ushambuliaji kuanza kuimarika hasa baada ya kurudi kwa Amisi Tambwe.

Akiongea na saluti5, Msuva alisema kurudi kwa Tambwe kumeimarisha safu ya ushambuliaji ambapo sasa akili yao ni ubingwa pekee.

Msuva alisema muunganiko kati yake, Tambwe na Obrey Chirwa kutaifanya sasa safu yao ya ushambuliaji kuwa tishio katika mechi zao.

Alisema, kwa sasa wanataka kuhakikisha wanamaliza tofauti ya mabao kati yao na Simba ambapo hilo litawasaidia katika mbio za ubingwa msimu huu.

“Unajua hapa kati kulikuwa na mambo mengi, kuna wenzetu walikuwa majeruhi lakini sasa wameanza kurudi, mfano Tambwe ambaye kurudi kwake kutaiongezea nguvu timu katika upande wa mabao,” alisema Msuva.


“Unajua Ligi ilipofikia kila kitu kinatakiwa kiende kwa mahesabu, kwanza ujue tujue kuongeza upana kwa kuwaacha Simba kwa mabao, tunapokuwa mimi, Tambwe na Chirwa hii ni ishara mbaya kwa wapinzani.”

No comments