MSUVA AWAHAKIKISHIA WANA YANGA USHINDI DHIDI YA PRISON JUMAMOSI

KINARA wa ufungaji kwenye michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simon Msuva amesema kuwa watahakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Prison ili kutimiza azma yao ya kutetea makombe yote mawili msimu huu.

Nyota huyo mwenye jumla ya mabao 12 kwenye orodha ya wafungaji hapa nchini, amesema kuwea dhamira yao ni kuhakikisha wanatetea mataji yote mawili ambnayo waliyabeba msimu uliopita.

“Watu wanadhani tumekata tamaa baada ya kupoteza mechi ya Shirikisho ugenini lakini nikuhakikishie kuwa dhamira yetu ya kutetea makombe yote mawili iko pale pale,” alisema Msuva.

“Hatuoni ni kipi cha kutuzuia kufikia malengo yetu mwishoni mwa msimu huu maana mpaka hivi sasa milango yote ipo wazi.”


Yanga inatarajia kukutana na Prisons ya Mbeya kwenye mchezo wa Kombe la FA Jumamosi wiki hii kwenye dimba la uwanja wa taifa, jijini Dar es Salaam.

No comments