MTUNZI WA MASHAIRI YA MIPASHO BONGO AKIRI KUSHUKA KWA MUZIKI WA TAARAB

MTUNZI nguli wa mashairi ya taarab, Al-hatib Job amekiri kuwa muziki huo umepoteza msisimko kwa kiasi kikubwa huku akisema kuwa hali hiyo imechangiwa zaidi na kuhamahama kwa wasanii lililotokea kwa “vurugu” kipindi cha kati.  

Akiongea na saluti5, Al-hatib alisema kuwa, ni kawaida kwa mtindo yote ya muziki kupanda na kushuka kulingana na upepo, lakini kwa upande wa taarab hilo limetokana na wasanii kuhama na hivyo kuwayumbisha na kuwapoteza mashabiki wao.

“Lakini kwangu naona huu ni wakati mgumu wa mpito tu ambao watu wa taarab wanaupitia na nadhani hali itakuwa shwari muda si mrefu, hasa kwa wasanii wenyewe kutulia na kuachia kazi nzuri,” amesema mtunzi huyo.


Amesema kuwa, mashabiki mara nyingi ni rahisi mno kudanganyika na kusahau yaliyotokea nyuma, hivyo anaamini iwapo wasanii watatuliza vichwa vyao na kufanya kazi kikamilifu, kuna uwezekano mkubwa wa kuipandisha upya taarab na kuirudisha kwenye ubora wake.

No comments