Habari

MUZIKI WA HERRERA USIPIME, MAN UNITED YALIPA KISASI KWA CHELSEA …Mourinho ni noma

on

Kiungo  Ander Herrera amedhihirisha kuwa ni kiungo bora baada ya kuizima kabisa Chelsea eneo la kiungo wakati Manchester United ikishinda 2-0 kwenye mchezo wa Premier League ulichezwa Old Trafford.
Herrera alimfunika Eden Hazard na kuhakikisha haleti madhara kila anapogusa mpira, lakini pia alifanya kazi kubwa ya kusambaza mipira kwa pasi za uhakika.
Kiungo huyo wa Hispania akatengeneza bao la kwanza lililofungwa na Rashford dakika ya 7 kabla yeye mwenyewe hajafunga goli la pili dakika ya ya 49.
Jose Mourinho akafanikiwa kulipa kisasi kwa timu yake ya zamani ambapo alitengeneza mfumo uliofanya Chelsea isimpe majaribu ya maana kipa David De Gea.
Kocha huyo akawaduwaza Chelsea kwa kumwanzisha benchi Ibrahimovic na kumchezesha Rashford kama mshabuliaji pekee.
Rashford  aliwachosha mabeki Zouma, David Luiz na Cahill kwa kuwakimbiza kila upande wa lango lao.
Manchester Utd: de Gea, Valencia, Bailly, Rojo, Darmian, Fellaini, Ander Herrera, Pogba, Lingard (Carrick 60), Rashford (Ibrahimovic 83), Young (Fosu-Mensah 90). 
Chelsea: Begovic, Zouma (Loftus Cheek 83), Luiz, Cahill, Moses (Fabregas 54), Kante, Matic (Willian 66), Azpilicueta, Pedro, Hazard, Costa. 
 Rashford  akiifungia United bao la kwanza
Herrera akishangilia bao lake

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *