MWANAMUZIKI HUYU ANATOA TASWIRA GANI KWA ‘MITUNGI’ HII YA MWENDO KASI?


Hii ni picha mwezi Machi mwaka huu, Jumapili fulani katika mji wa Dodoma ndani ya ukumbi wa Victoria Pub.

Pichani ni mwanamuziki mwenye vidole hatari kwa kuchambua nyuzi za gitaa la solo na rhythm, kwa jina anajulikana kama Amos Nabii aliyepata kutamba na bendi za Bambino, Vibration Sound, Mashujaa Band na Twanga Pepeta.

Hapo ni wakati anaitumikia bendi ya Sky Melodies ya Dodoma ambapo wakati wenzake wanapiga kazi, yeye alikuwa anauchapa usingizi ukumbini kutokana na matumizi ya pombe yaliyopitiliza.

Amos amekuwa mmoja wa wanamuziki wanaopiga sana ‘kilaji’ na moja ya matukio ambayo Saluti5 iliyashuhudia ni pale alipofanya vurugu za kilevi hadi kutolewa nje kwenye mkutano wa wanamuziki wa dansi na mheshimiwa Nape Nnauye mwaka jana kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall.

No comments