NAVY KENZO WATUA ISRAEL KUNADI ALBAMU YAO MPYA YA "AIM"

KUNDI la muziki La Navy Kenzo ambalo linaundwa na wapenzi Aika na Nahreel limefanya ziara nchini Israel na kuitambulisha albamu yao mpya ya "AIM."

Kundi hilo ambalo limeonekana kufanya vYema kwenye tasnia ya muziki nchini, limetua Israel juu kwa ajili ya kufanya maonyesho ikiwa ni pamoja na kunadi albamu yao hiyo mpya.

Aika na Nahreel walikutana nchini India wakiwa masomoni na kuanzisha uhusiano wa kimapenzi kabla ya kuamua kuunda kundi la Navy Kenzo baada ya kuonekana wote wanapenda muziki.


Baada ya ziara hiyo kwenye jiji la Tel Aviv, Israel ambapo wamefanya onyesho kwenye ukuwa wa Brbie, watarejea Tanzania na kuzunguuka mikoani ili kuendelea kuinadi ablamu yao hiyo ya "AIM" yenye maana ya Above Inna Minute.

No comments