NEW AUDIO: MWENGE JAZZ “PASELEPA” YAJA KIVINGINE …sikiliza wimbo wao mpya kabisa “Heshima Yangu”
Moja ya bendi bora iliyowahi kutokea hapa nchini, Mwenge Jazz wana Paselepa au ukipenda iite Mwenge ya Mashujaa, imekuja kivingine baada ya ukimya wa muda mrefu.

Mwenge Jazz inashuka na wimbo mpya kabisa “Heshima Yangu” mtunzi akiwa ni binti mpya katika muziki wa dansi Leah Lyeme (pichani) ambaye ndiye ameimbisha wimbo huu kwa sehemu kubwa.

Ni wimbo mzuri ulioko kwenye miondoko ya kisasa, kazi ikiwa imezalishwa katika studio za Sound Crafters zilizoko Temeke, jijini Dar es Salaam.

Ndani ya wimbo huu wa dakika 5 na sekunde 29, utasikia namna wapiga ala wanavyopishana kifundi na ambapo solo limekung’utwa na Salum Dialo ambaye ndiye kiongozi wa bendi, bass ni mkono wake Profesa Kandaya, kinanda ni Japhet Makinda na  gitaa la kati limedonyolewa na Peter Mafwalo.


Drum zimepigwa na Abdallah Ally Bravo, tumba zimegongwa na Hamis Juma wakati saxaphone utakayoisikia imepulizwa na kijana mdogo kabisa Ezekiel Lumbagala.

Waimbaji walioshiriki wimbo huu mbali na Leah ni Shukuru Majaaliwa, Hussein Mtamile, Abdurahman Sangali, Athuman Hussein na Shazilu Omar.

Isikilize hapo juu ngoma hiyo mpya ya Mwenge Jazz "Heshima Yangu".


No comments