Habari

OKWI, KASEJA MBIONI KUREJEA SIMBA SC… wamo pia mastaa wengine watatu kutoka timu nyingine

on

SIMBA
imesikia kwamba baaadhi ya timu zimeanza kuwinda majina ya wachezaji wake
kuelekea usajili ujao wa Ligi Kuu msimu wa 2017/18 lakini haijali.
Badala yake
wekundu hao wa Msimbazi tayari wamejibu mapigo kwa staili yake baada ya kuwapa
mikataba ya awali wachezaji watatu matata waliofanya vyema kwenye Ligi Kuu ya
soka Tanzania Bara msimu huu.
Saluti5 inajua kwamba mastaa hao watatu ambao tunalazimika kuhifadhi majina yao kwa
sasa tayari wana uhakika mkubwa wa kuichezea Simba na mazungumzo yao na yamefikia patamu hivi sasa.
Katika uchunguzi wetu tumegundua kwamba wachezaji hao walikuwa jijini Dar es Salaam
wikiendi hii na wameshamalizana na mratibu anayeendesha mpango huo.
Wachezaji wanaotajwa kwamba wanaweza kusajiliwa Simba ni pamoja na Emanuel Okwi ambaye ni Mganda anayerejea Msimbazi kwa mara nyingine, kiungo wa Mbeya City, Kennny Ally
pamoja na mshambuliaji wa Kagera Sugar ambaye anacheza kwa mkopo kwenye timu
hiyo akitokea Simba Mbaraka Yusuf Abeid.
Lakini pia Simba wanadaiwa kufanya mipango ya kumrejesha kipa wake wa zamani, Juma Kaseja ambaye naye yuko Kagera Sugar na amekuwa katika kiwango kikubwa sana.

Hata hivyo habari zinasema kwamba mastaa watatu waliochinjwa jijini Dar es Salaam toka juzi
sio hao wanaotajwa mara kwa mara.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *