KIONGOZI wa Yah TMK Modern Taarab, Omary Teggo “Special One”, amesema kuwa, bosi wao, Said Fella hajawabwaga kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakisambaza uvumi huo.

Akiongea na Saluti5, Teggo amesema kuwa amezisikia tetesi hizo ambazo hata hivyo anadai kuwa zinasambazwa kwa makusudi na baadhi ya watu wasio na nia nzuri na bendi yao.

“Sisi bado tuko chini ya Mkubwa (Fella) na hilo yeye mwenyewe ameshalizungumza hata kwenye kituo kimoja cha radio, hao wanaoeneza taarifa za kizushi acha tu waendelee kwani hatuna budi nao,” amesema Teggo.

“Kwa kuthibitisha zaidi ni kwamba, hivi sasa Fella anashughulikia suala la vyombo vyetu vipya vya muziki alivyotuagizia kutoka nje ya nchi ambavyo vinatarajiwa kutua muda si mrefu,” aliongeza Teggo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac