OMOTOLA JALADE ASEMA ILIMCHUKUA MUDA MREFU "KUMSOMA" MUMEWE KABLA KUKUBALI KUOLEWA NAE

STAA wa filamu nchini Nigeria, Omotola Jalade ameweka wazi kuwa ilimchukua muda mrefu kutafakari kabla ya kufunga ndoa na Ekeinde ambaye ni rubani wa ndege.

Mrembo huyo ambaye hivi karibuni alikuwa kwenye ziara ya nchi za Morocco na Ghana ambako alipata wasaa wa kuzungumza na wananchi wa chuo kikuu cha Biachala, alisema kuwa alijiona bado mdogo kuweza kukabiliana na mikikimikiki ya ndoa.

“Nilihisi bado sijakomaa kuweza kukabiliana na changamoto za ndoa nilipokuwa msichana mpaka lilipotoka shinikizo la ndugu zangu waliokuwa sambamba na mchumba wangu,” alisema Omotola.

“Baada ya kuingia rasmi katika maisha ya ndoa naona kila kitu kinakwenda sawa, bado sijakumbana na magumu katika maisha yangu kiasi cha kunifanya nijute,” aliongeza mrembo huyo.

Staa huyo wa filamu alipokuwa nchini Ghana alipata kukutana na mke wa rais mama Rebecca Akufoka Addo kabla ya kuzuru kwenye vyuo vikuu.

No comments