Habari

OZIL PASUA KICHWA EMIRATES …ARSENAL KUAMUA KUSUKA AU KUNYOA

on

Mesut Ozil bado ni pasua kichwa Arsenal juu ya hatma yake baada ya kuendelea kuuchunia mkataba mpya uliowekwa mezani.
Ozil aliyenunuliwa kutoka Real Madrid kwa pauni milioni 42, ni mmoja wa wachezaji wanaolipwa mshahara mkubwa Emirates akiwa anapokea pauni 140,ooo kwa wiki, lakini amesita kusaini mkataba mpya utakaomfanya alipwe pauni 250,000 kwa wiki.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani, anatajwa kuwaniwa na timu kadhaa zikiwemo ofa nono kutoka China.
Hata hivyo watu wa karibu na Ozil mwenye umri wa miaka 28 wamedai mshambuliaji huyo hana mpango wa kwenda kucheza mashariki ya mbali.
Mkataba wa sasa wa Ozil unaisha mwishoni mwa msimu ujao na kama ataendelea kudengua kusaini mkataba mpya, itabidi Arsenal wampige bei kiangazi hiki ili asiondoke bure miezi 13 ijayo.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *