P-SQUARE WAJA NA KIBAO KIPYA CHA "NOBODY UGLY"

MARAPA pacha wanaounda kundi la P-Square ambao waliripotiwa kuwa katika bifu la wao kwa wao, hivi sasa wameachia wimbo ya “Nobody Ugly".

Tayari wamekamilisha video ya wimbo huo na hivi karibuni wamepanga kuirusha mtandaoni.

Katika wimbo huo, Peter na Paul wamejaribu kuelezea namna ambavyo mitandao ya kijamii inapotosha umma kwa kiasi kikubwa ambapo mambo mengi yanayoelezwa huwa hayana ukweli wowote.


Peter na Paul waliunda kundi la P-Square ambalo limejipatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya Afrika lakini baadae waliingia kwenye malumbano huku kila mmmoja akipania kufanya kazi peke yake.

No comments