PATACHIMBIKA TRAVERTINE JUMAPILI HII, WAKALI WATANO NA BENDI ZAO TANO JUKWAA MOJA … Ni nani mkali zaidi ya mwenzieJumapili hii kutakuwa na mchuano mkali wa waimbaji nyota watano wa muziki wa taarab ndani ya ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Lakini kama vile hiyo haitoshi, waimbaji hao watapigiwa ‘live’ na bendi zao na hapo ndipo utamu utakapozidi kunoga.

Fatma Mchauruko wa Yah TMK, Khadija Yussuf wa Wakali Wao, Hanifa Maulid “Jike la Chui” akiwa na Funga Kazi, Mwamvita Shaibu kutoka Ogopa Kopa na Mwasiti Kitoronto wa Jahazi wataumana kutafuta nani mkali zaidi ya mwenzie.

Malkia wa Mipasho Bi Khadija Kopa na mfalme wa Kibao Kata Kivurande watasindikiza mpambano huo wa aina yake.

Inakuweje zinapokutana Jahazi, Wakali Wao, Ogopa Kopa, Yah TMK na Funga Kazi? Nenda Travertine Jumapili hii April 30.

No comments