Habari

PAUL SCHOLES ASEMA MARCUS RASHFORD NI ANGA ZA CRISTIANO RONALDO NA NEYMAR

on

Kiungo wa zamani wa Manchester United, Paul Scholes amesema  mshambuliaji kinda wa klabu hiyo, Marcus Rashford ana vigezo vyote vya kufikia uwezo  Cristiano Ronaldo na  Neymar. 
Rashford amefunga magoli 10 katika mechi 44 msimu huu na sasa Paul Scholes anaamini kinda huyu atakuwa mmoja wa washambuliaji bora duniani. 
“Rashford atakuwa mshambuliaji bora, hakuna shaka juu ya hilo,” Scholes aliiambia BBC Radio 5 Live. “Kasi yake ni ya maajabu. Ni mchezaji bora klabuni akiwa na umri wa miaka 19 tu.
“Tulichokiona kwake katika mchezo dhidi ya Anderlecht ni kasi ya ajabu, uwezo na mbinu za kuwapita wachezaji pinzani kama vile hawapo uwanjani”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *