PICHA 30: MWILI WA SAMWEL MSHANA ULIVYOAGWA DAR ES SALAAM …Simanzi yatawala CCM Mwinjuma


Nyuso za huzuni, zimanzi pamoja na vilio vilitawala ndani ya ukumbi wa CCM Mwinjuma Jumatatu mchana wakati mwili wa mpiga bass wa TOT Samwel Mshana ulipokuwa ukiagwa.

Mshana alifariki Jumamosi alfajiri katika hospitali ya taifa Muhimbili na atazikwa Jumanne mchana nyumbani kwao Makanya mkoani Kilimanjaro.


Zifuatazo ni picha 30 za namna mwili wa Samwel Mshana ulivyoagwa na watu wengi wakiwemo wasanii wa bendi mbali mbali.
 Wasanii wa TOT wakiimba wimbo maalum wa maombolezo
 Sehemu wa watu waliofika CCM Mwinjuma kuuaga mwili wa Samwel Mshana
 Malkia Khadija Kopa alishindwa kujizuia
 Ilibidi Khadija Kopa akapumzishwe kwa muda ndani ya ofisi za TOT
 Waombolezaji wakiwa CCM Mwinjuma
 Sanduku lililohifadhi mwili wa Samwel Mshana
 Katikati mwenye nguo nyeupe ni mzazi mwenzake na Samwel Mshana akiwa na mtoto wao
 Ismail Sumaragar swahiba wa marehemu akifarijiwa na mkewe
 Nyuzo za huzuni zilitawala kwa wasanii wa TOT
 Sumaragar akiongoza zoezi zima la shughuli ya kuaga mwili wa Samwel Mshana
 Ni wasaaa wa kusomewa wasifu wa marehemu
 Kushoto ni mwimbaji mkongwe wa TOT Ally Star
 Hali ilivyokuwa ukumbini
 Wadau na wanamuziki wengi walijitokeza
 Mkurugenzi wa TOT Gasper Tumaini akitoa neno la shukrani
 Kulia ni mwimbaji Saleh Kupaza wa Ivory Band
 Waimbaji wa Vijana Jazz Saburi Athuman na Abdallah Mgonahazilu
 Wasanii wa maigizo na muziki wakiwa ukumbini
 Baadhi ya wasanii waliofika kuaga mwili wa Samwel Mshana
 Huzuni tele
 Taswira ya ukumbi wa CCM Mwinjuma 
 Mzazi mwenzake na marehemu akiaga mwili wa kipenzi chake
 Hakika ilikuwa ni simanzi tele
 Binti wa marehemu akifarijiwa
 Mwili ukitolewa nje kupelekwa kwenye gari tayari kwa safari ya kuelekea Makanya
 Nje ya ukumbi wa CCM Mwinjuma
 Mwili unapandishwa kwenye gari
 Mwili wa Samwel Mshana unaingia ndani ya gari
Mwili wa Samwel Mshana  tayari umewekwa ndani ya gari

No comments