PICHA 8: MSONDO NGOMA WAANZA RASMI BURUDANI EQUATOR GRILL... mashabiki wachizika na "Kauka Nikuvae", "Penzi Kizungumkuti", "Mwana Mkiwa"

WAKONGWE wa muziki wa dansi, Msondo Ngoma Music Band jana walianza rasmi kutifua burudanbi ndani ya ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam watakakokuwa wakidondoka kila wiki katika siku za Alhamisi.

Saluti5 kama kawaida ilihudhuria shoo hiyo kuanzia mwanzo hadi mwisho na kushuhudia namna mashabiki waliofika wakicharuka kati kucheza na wengine kupanda jukwaani kuwatuza wasanii walioonekana kuwakosha zaidi.

Vibao vingi vipya na vya zamani, vikiwemo vile vya “Kauka Nikuvae”, “Penzi Kizungumkuti” na “Mwana Mkiwa”, vilionekana kushitua zaidi nyoyo za wapenzi ambao walikuwa wakilazimika kuviacha viti vyao vikiwa tupu kila nyimbo hizo zilipoporomoshwa.

Picha 8 chini zinaonyesha namna Msondo Ngoma walivyokinukisha ndani ya ukumbi huo:
 Waimbaji Eddo Sanga (kushoto) na Juma Katundu wakimwaga raha kwa wapenzi wao
 Mcharazaji gitaa zito la Bass, Davido Bass akisisimua mashabiki wa Msondo Ngoma
 "Mkaanga Chips" James Mawila akifanya yake
 Eddo akiimba kwa bashasha za hali ya juu
 Roman Mng'ande "Romarii" akiongeza ladha jukwaani kupitia ala yake ya Tarumbeta
 Safu ya waimbaji vijana wa Msondo Ngoma, kutoka kushoto ni Hassan Moshi, Athuman Kambi, Eddo Sanga na Juma Katundu
Hapa Abdul Ridhiwan "Pangamawe" akiwajibika
Zahor Bangwe akiungurumisha gitaa la Kati la Rythm kwa ufundi mkubwa

No comments