PIERRE AUBAMEYANG ATABIRIWA KUVUNJA REKODI YA USAJILI YA PAUL POGBA

UTAFITI uliofanywa na vyombo vya habari nchini Ujerumani umempa alama nyingi mshambuliaji wa Borrusia, Pierre Aubameyang kuvunja rekodi ya uhamisho iliyowekwa na Paul Pogba ambaye ndiye mchezaji ghali hivi sasa kutokana na uhamisho wake wa kutoka Juventus kwenda Manchester United.

Inakadiriwa Aubameyang atauzwa dau lisilopungua mil 100 wakati wa majira ya kiangazi baada ya dirisha kubwa la usajili kufunguliwa mwishoni mwa msimu huu.


No comments