PIGA UA, WENGER ATAKE ASITAKE, ARSENAL LAZIMA IAJIRI MKURUGENZI WA SOKA MSIMU UJAO


Arsenal inatarajiwa kuajiri mkurugenzi wa soka ili kuepuka mikanganyiko ya mikataba ya wachezaji iliyogubika klabu hiyo msimu huu.

Alexis Sanchez na Mesut Ozil wanaingia kwenye miezi 12 ya mwisho ya mikataba yao, hatua inayomaanisha kuwa wanaweza wakasaini mkataba wa awali wa usajili huuru kwenda klabu yoyote mwezi Januari.

Hali ipo hivyo pia kwa Alex Oxlade-Chamberlain, Kieran Gibbs na Jack Wilshere.

Arsenal inamtaka mkurugenzi wa soka ili pamoja na mambo mengine, lakini awe pia  mtendaji mkuu mwenye sauti ya mwisho katika nyendo za usajili na mikataba ya wachezaji. 

Wenger amekuwa mtu pekee mwenye mamlaka ya soka klabuni tangu alipojiunga nayo miaka 21 iliyopita - akiwa na kauli ya mwisho juu ya usajili na mustakabal wa mikataba ya wachezaji.

Hatua ya kuajiri mkurugenzi wa soka inaaminika ni hatua ambayo haitapokewa vema na Wenger, lakini klabu hiyo inahisi kuwa bosi huyo ameelemewa na anahitaji msaada.

Mapema mwezi huu mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Marc Overmars alitajwa kama mtu mwenye nafasi kubwa  zaidi ya kushika nafasi hiyo.


Overmars ambaye kwa sasa ni mkurugenzi wa soka wa  Ajax, aliitumikia Arsenal kwa miaka mitatu na kushinda mataji ya Premier League na FA Cup chini ya Wenger mwaka 1998.

No comments