Habari

PIGO! CHELSEA KUMKOSA KIPA THIBAUT COURTOIS DHIDI YA MAN UNITED

on

Chelsea imepata pigo kuelekea mechi yao dhidi ya Manchester United kwa kumkosa kipa   chaguo la kwanza Thibaut Courtois.
Kipa huyo aliumia kifundo cha mguu mazoezini na sasa Daily Mail la Uingerza linaandika kuwa hataweza kucheza mechi hiyo itakayopigwa Old Trafford.
Thibaut Courtois amekuwa mhimili mkubwa kwa sehemu ya ulinzi ya kikosi cha Antonio Conte na bila shaka Manchester United watapokea vizuri habari za kukosekana kwake.
Kipa huyo wa kimataifa wa Ubelgiji amecheza mechi 31 za Premier League msimu na kutoka bila kufungwa (clean sheets) mara 13.  
Kipa namba 2 Asmir Begovic anatagemewa kucheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu msimu huu. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *