PLUIJIM AKANA KUWA NA MPANGO WA KUMSAJILI HARUNA NIYONZIMA SINGIDA UNITED

KOCHA wa timu ya Singida United, Hams Pluijim anaonekana kuigeukia timu ya Yanga baada ya kuhusishwa na mpango wa kumnasa kiungo Mnyarandwa, Haruna Niyomzima mwishoni mwa msimu huu.

Jina la Niyomzima lipo kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na Plujim kwa ajuli ya kuimarisha kikosi chake kulichopanda daraja.

Niyomzima ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alisita kuthibitisha taarifa hizi zaidi ya kudai kuwa mpango wake ni kutimkia Rwanda kupumzika baada ya Ligi kuisha.

“Kwanza nataka kuhakikisha Yanga inatetea mataji yote iliyobeba na baada ya msimu kuisha nitaenda Rwanda kupumzika kabla sijahamua wapi nitatimkia," alisema Niyomzima ambaye amekaa Yanga kwa miaka sita.

“Nikweli mkataba wangu unaisha Yanga mwishoni mwa msimu huu lakini ni mapema sana kuweka wazi juu ya mipango yangu ya baadaye ukizingatia bado tupo kwenye michuano ya Ligi na Kombe la FA,” aliongeza kiungo huyo.


Hansa Plujim anahusishwa kutaka kumnasa kiungo huyo ili kukitia moyo kikosi chake ambapo pia kocha huyo alikuwa na maelewano mazuri na Niyomzima tangu alipokuwa Yanga.

No comments