PLUIJIM APANGA KUONGEZA WACHEZAJI WAWILI WA KIMATAIFA SINGIDA UNITED ILI KUIPA MAKALI ZAIDI

KOCHA mpya wa timu ya Singida United, Hans Plujim amepanga kuongeza wachezaji wengine wawili wa Kimataifa ili kukitia makali kikosi chake kabla ya kuanza msimu kwa mpya wa ligi kuu Tanzania Bara.

Pluijim ambaye hivi karibuni aliwatambulisha nyota wapya kutoka Zimbabwe ambao Elisha Muroiwa na Wisdom Mtasa amepanga kuongeza wengine wawili ili kujiwinda kwa msimu kwa msimu ujao.

Singida United tayari imesajili jumla ya wachezaji watatu wa kigeni kwenye kikosi chake huku ikiwa na mipango ya kuongeza wengine wawili ili kufikia eatano ambapo kanuni za Soka za TFF zinaruhusu wachezaji saba.

“sisi bado ni timu change hivyo tumepanga kusajili jumla wachezaji watano wa kigeni na siyo saba kama sheria inavyoruhusu.

Nimatarajio yetu kuwapa nafasi zaidi wachezaji wa ndani katika mechi za Ligi kuu” alisema katibu mkuu wa klabu hiyo, Abdulrahman Sima.

“Tumefanikiwa kupanda daraja tunataka kuionyesha Tanzania kile ambacho tunaweza kukifanya kwa kuleta upinzani wa kweli na siyo kushiriki kwa mazoea kama ambavyo vilabu vingine huwa vinafanya”, aliongeza katibu huyo.


Baada ya kupanda daraja,Singida United ilimnasa aliyekuwa Mkurugenzi wa benchi la Ufundi la Yanga, Hans Pluijim raia wa Uholanzi ili kukipa uzoefu kikosi hicho.

No comments