POBGA AMPIGIA SALUTI N'GOLO KANTE WA CHELSEA


Mchezaji ghali duniani Paul Pobga amempigia saluti kiungo wa Chelsea N'Golo Kante na kusema ni mchezaji bab kubwa.

Pobga ambaye Jumapili hii atakuwa na kibarua kingine cha kukabiliana na Kante wakati Manchester United itakapoikaribisha Chelesea kwenye mchezo wa Ligi Kuu, ameiambia MUTV kuwa Kante anahaha uwanja mzima.

"Ni mmoja wa wachezaji bora kwa Chelsea. Analeta utofauti kwa sababu unapoona timu yake inapoteza mipira, anaweza akapoteza mara tatu lakini akapora mipira mara nne.

"Yupo kila sehemu uwanjani, ni mchezaji mkubwa," alisema Pobga.

No comments