Habari

PSG YAUNGANA NA CHELSEA KUWANIA SAINI YA ALEXIS SANCHEZ

on

Paris Saint-Germain imeungana na Chelsea katika mbio za kusaka saini ya mshambuliaji wa Arsenal, Alexis Sanchez.
Mabingwa hao wa Ufaransa wanataka Sanchez aungane na Edinson Cavani na Angel di Maria na kuunda safu hatari ya ushambuliaji ili kuwa na makali ya kutosha kwenye Champions League msimu ujao.
Sanchez mwenye umri wa miaka 28 amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, jambo linalotoa sura kuwa Arsenal itakuwa tayari kumpiga bei kuliko aondoke bure iwapo atamalizia mkataba wake Emirates.
Chelsea tayari imeonyesha uchu wa kutaka huduma ya Sanchez lakini ni wazi kuwa Arsenal itachagua kuumuza nje ya England ili kuepuka kumuuzia ‘silaha adui’. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *