RAMADHANI SINGANO ASEMA WATAHAKIKISHA AZAM WANATWAA KOMBE LA FA

BAADA ya kujihakikishia namba kwenye kikosi cha Azam, mshambuliaji wa timu hiyo, Ramadhan Singano amesema kuwa hivi sasa wamepania kuhakikisha wanabeba Kombe la FA ili wapate tiketi ya kuendelea kushiriki kwenye michuano ya kitaifa msimu ujao.

Singano ambaye amefanikiwa kuifungia Azam mabao matatu ndani ya mechi nne zilizopita, amesema kuwa baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali wamefufua matumaini ya kushiriki michuano ya kitaifa, hivyo hawahofii timu yoyote watakayocheza nayo.

“Hakuna sababu itakayofanya tukose tiketi ya kushiriki michuano ya kitaifa kwa sababu hivi sasa tumeelekeza nguvu zetu kwenye Kombela FA ili kunasa tiketi ya kwenda CAF,” alisema nyota huyo aliyewahi kuitumikia Simba akaondoka kwa mizengwe.

“Hakuna timu tunayoihofia hivi sasa, kama tutakutana tena na Yanga FA kunaweza kukawepo na upinzani mkali kama ilivyokuwa kwenye mechi ya Ligi ambapo tulipoteza kwa bao 1-0,” aliongeza nyota huyo.

Azam imepoteza matumaini ya kubeba ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na nafasi pekee ya kushiriki michuano ya kimataifa ni kuhakikisha wanabeba ubingwa wa Kombe.

No comments