RAMSEY NOAH ASEMA "MAPENZI MUBASHARA" ANAYOYAONYESHA KWENYE MUVI HAYALETI HISIA MBAYA KWA MKEWE

STAA wa Nollywood, Ramsey Noah amesema kwamba filamu zote za mapenzi ambazo amekuwa akitengeneza, hazijawahi kuleta matatizo kwenye ndoa yake iliyodumu kwa miaka 15.

“Mke wangu anafahamu kazi yangu ni kucheza filamu na kuna wakati nacheza filamu za mapenzi, hili ni suala ambalo liko wazi kwake na halimpi taabu kama ambavyo watu wanaweza kudhania,” alisema staa huyo.

“Ndio kuna baadhi ya maeneo ni magumu kuigiza, kama vile kukumbatiana na kupigana mabusu, lakini ninapaswa kufanya hivyo kwasababu hii ni sanaa ya maigizo na sio jambo rahisi,” aliongeza Ramsey.


“Nashukuru kwa kuwa mke wangu amekuwa akiniunga mkono kwa kila jambo ambalo nimekuwa nalifanya kupitia sanaa.”

No comments