RAPA BILL NASS AAMUA KUMFICHA MPENZI WAKE KUOGOPA "MAJANGA" YALIYOWAHI KUMTOKEA

RAPA Bill Nass amefunguka sababu ya kutoweka wazi mahusiano yake na kwamba kamwe hatomwanika mpenzi wake na amefunguka sababu inayomfanya awe hivyo.

Akiongea na kipindi cha Bongo.com cha radio Time Fm, amesema alishawahi kuwa katika mahusiano mengi ambayo hakuwa na bahati nayo.  

“Nimekuwa kwenye mahusiano mengi ambayo sikuwa na bahati nayo, pia inaweza kukutengeneza kisaikolojia kutokana na mambo ambayo nayaona kwa rafiki zangu. Nina bahati ya kuona hivyo vitu kwahiyo sijui huko mbele,” amesema rapa huyo.


Bill ameongeza kuwa kwa sasa hana mahusiano na mrembo yeyote wala hajawahi kufikiria kuoa hivi karibuni.

No comments