Habari

REAL MADRID YATAKATA BILA BENZEMA, BALE NA RONALDO … Isco shujaa Sporting Gijon ikipigwa 3-2

on

Ikicheza bila nyota wake watatu BBC – Benzema, Bale na Cristiano Ronaldo, Real Madrid ikaibanjua Sporting Gijon 3-2 na kuzidi kujikita kileleni mwa La Liga.
Hata hivyo Real Madrid ililazimika kutoka nyuma mara mbili kwa timu hiyo inayoshika nafasi ya 18 ambayo ilitangulia kufunga dakika ya 14 mfungaji akiwa Mikel Vesga lakini Isco akachomoa dakika tatu baadae.
Sporting Gijon wakatangulia tena kwa bao la Mikel Vesga dakika ya 50 lakini Alvaro Morata  akasawazisha dakika ya 59 huku Isco akiifungia Real Madrid bao la ushindi dakika ya 90.
SPORTING GIJON: Cuellar; Lillo, Mere, Babin, Amorebieta, Lopez; Carmona, Alvarez (Afif 90), Vesga, Gomez (Cases 69); Cop (Ndi 79).
REAL MADRID: Casilla; Danilo, Sergio Ramos, Nacho, Coentrao (Marcelo 57); Isco, Kovacic (Casemiro 89), Rodriguez; Vazquez (Mariano 71), Morata, Asensio.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *