REHEMA TAJIRI AMMIMINIA SIFA LUIZA MBUTU KWA KUDUMU MUDA MREFU TWANGA PEPETA

MWIMBAJI nguli wa kike kutoka The African Stars Band “Twanga Pepeta”, Luiza Mbutu amemiminiwa sifa kemkemu kwa kumudu kudumu ndani ya bendi hiyo tangu ilipoanzishwa.

Sifa hizo zimetolewa na mmoja wa wanamuziki wenzie wa kike, Rehema Tajiri katika mazungumzo maalum na Saluti5, ambapo amesema kuwa kwa kawaida ni nadra wasanii wa kike kuwa watulivu kwa kiasi cha Luiza.

“Kiukweli namsifu sana, kwani ameonyesha mfano bora kwetu sote na kutuamsha kiakili,” amesema mwanadada huyo ambaye hivi sasa anatamba na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la “Hafai”.


Luiza ambaye ni mke wa mwanamuziki mkongwe Faliara Mbutu, ndie msanii pekee aliyebakia Twanga Pepeta ambaye yuko na bendi hiyo tangu ilipoanzishwa rasmi mwishoni mwa miaka ya 90.

No comments