REHEMA TAJIRI ATOA SOMO ZITO KWA WASANII WA FILAMU BONGO... ammiminia sifa Tecla Mjata kwa kutokuwa na majivuno

WASANII wa filamu Bongo wameshauriwa kuanza kuandaa kazi zitakazowavutia mashabiki na kuwafanya wasahau habari za Tamthilia za kutoka nje ya nchi na kurudisha mawazo yao katika muvi za nyumbani.

Ushauri huo umetolewa na nguli wa kike wa muziki Bongo, Rehema Tajiri katika mazungumzo maalum na saluti5 ambapo amesema kuwa, kuna mapungufu mengi katika sanaa ya filamu hapa nchini yanayosababisha kupoteza msisimko kwa watazamaji.

“Tofauti ya sanaa ya zamani ambapo wasanii walikuwa wanajitambua, walikuwa na heshima na ubora wao ulikuwa uko juu, hivi sasa waigizaji wengi ni wauza sura tu ambao aidha wameingia kwenye fani hiyo baada ya kukosa shughuli ya kufanya au kwa kutafuta kujulikana,” amesema Rehema.

Rehema ambaye alishawahi kucheza michezo miwili katika runinga ya ITV wakati wa uhai wa baba yake aliyekuwa anajulikana zaidi kwa jina la “Mzee Janja”, amesema wasanii wa zamani walikuwa wanaigiza maisha halisi tofauti na sasa.


“Wasanii wakina mama walikuwa wanajielewa, hawakuwa watu wa sifa, walikuwa ni watu wa watu wote na walikuwa wakijishusha ili kila mtu awafikie na mfano wa wasanii hao ni mama yangu Tecla Mjata ambaye hadi leo anaishi mfumo wa kizamani wa kutokuwa na majivuno.”

No comments