REHEMA TAJIRI AWAANIKA WAKONGWE WA MUZIKI WALIOMNOA KATIKA UIMBAJI

MWANAMUZIKI Rehema Tajiri anayetamba sasa na kibao cha singeli cha “Hafai”, amefichua kwamba amepitia mafunzo ya wakongwe wengi wa muziki wa dansi hadi kufikia pale alipo.

“Baadhi ya wakongwe hao ni Hassan Rehani Bitchuka, Benno Villa Antony, Shaaban Dede, Mohammed Mwinyikondo, Huseein Jumbe pamoja na marehemu Muhiddin Gurumo,” amesema.

Amesema kuwa anakumbuka kuwa “Chichi Dchichambe” ni kati ya nyimbo zake za kwanza kujifunzia muziki wakati huo, huku akibainisha kwamba marehemu Tabia Mwanjerwa alikuwa chachu ya yeye kujikita katika fani ya uimbaji.


Rehema anayemtaja marehemu “De La Chance” kuwa ni kati ya watu waliokuja kumnyoosha palipobakia kwenye uimbaji wake, amesema kwamba, tofauti na wanavyodhani wengi, wakati yuko na Max Bushoke alikuwa bado hajaanza muziki.

No comments