REHEMA TAJIRI AWOMBA MAPROMOTA KUJITOKEZA KUFANYA NAE KAZI BILA KUHOFIA “UZEE” WAKE

MWANAMUZIKI wa kike, Rehema Tajiri ameibuka na kusema kuwa anatafuta promota wa kumsimamia huku akisisitiza kutomuogopa kutokana na umri wake.

“Pengine mapromota watahofia kuwa sitaweza tena kufanya chochotye kutokana na umri, lakini nawahakikishia kuwa hilo si tatizo, ndio maana mtu kama mama Khadija Kopa pamoja na umri alionao lakini bado anakamua,” amesema.

Anawaomba mapromota wamwite wafanye nae kazi akisema kwamba, kutokana na mustakabali wa maisha ya kikuziki kwa sasa, ni vigumu msanii kujiendesha mwenyewe bila ya kuwa na “menejimenti”.

Amesema, anahitaji kuwa na menejimenti ili aweze kuwafikia mashabiki na kumudu promo za media ambazo kwa madai yake, hawezi kufanikiwa bila ya kuwa na nguvu ya ziada kutoka kwa msimamizi.

Amewaahidi mashabiki kuwa amerudi upya kwenye gemu, hasa baada ya hivi karibuni kuingia Studio za Mo Fire na kuachia kibao kipya cha miondoko ya “Singeli” kiitwacho “Hafai” ambacho kinaendelea kutesa.


Akizungumzia zaidi kimya chake kwenye gemu, Rehema ambaye ni mtoto wa alkiyekuwa nguli wa maigizo ya runinga, Hamis Tajiri, amesema kuwa  aliamua “kupotea” kwa makusudi kwa miaka mitano sita ili kupotezea maneno ya watu waliokuwa wanadai ameisaliti ndoa yake kwa ajili ya muziki.

No comments