Manchester United imekumbwa na balaa lingine la majeruhi baada ya sentahafu wake tegemeo Marcos Rojo kuumia na kutolewa nje kwa machela kwenye mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht.

Beki huyo wa  Argentina aliumia goti la kushoto dakika ya 20 tu kwenye mechi hiyo iliyochezwa Old Trafford na hakuweza kuendelea.

Picha zilionyesha Rojo alikuwa akiomba dua wakati akitolewa na machela huku nafasi yake ikichukuliwa na Daley Blind.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac