ROMA MKATOLIKI ASHAURIWA KUSAHAU TUKIO LA KUTEKWA NA KUGANGA YAJAYO

RAPA Bill Nass amemtaka mwanamuziki mwenzie wa Bongofleva Roma Mkatoliki kusahau tukio la kutekwa na na upiga kazi yake ya muziki kama kawaida.

Akizungumza na saluti5, Bill Nass alisema kuwa hakuna haja ya kuumizwa na suala ambalo limeshapita badala yake anapaswa kuganga yajayo kwa faida yake.

Bill ambaye amewahi kutamba na wimbo wake wa "Mazoea" aliongeza kuwa Roma Mkatoliki na mwenzake ambao walikumbwa na mkasa wa kutekwa kwenye Studio za Twonga Records wanapaswa kupiga kazi.

“Ni jambo la kushukuru Mungu kwa kuwa wapo hai hadi leo lakini wanapaswa kuachana na mawazo yaliyopita na kuendelea kufanya kazi ya sanaa kama kawaida,” alisema rapa huyo.


“Ukiendelea kuwaza kilichopita huwezi kuwa bora kwa jambo lijalo hivyo wanatakiwa kuachana kabisa na suala lililo wakuta” aliongeza.

No comments