RONALD KOEMAN amefichua kuwa Romelu Lukaku amemweleza kwamba hata saini mkataba mpya Everton. 
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ubegiji kwa sasa ndiye kinara wa upachikaji mabao kwenye Premier League akiwa ameshaifungia Everton magoli 23 msimu huu.
Hata hivyo, pamoja na mafanikio hayo, Lukaku hana mpango wa muda mrefu wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo.
Lukuku ameshakataa kurefusha mkataba wake Goodison Park na sasa amemwambia kocha wake kuwa mpango huo haupo kabisa kwenye fikra zake.
"Ameniambia kuwa hatasaini mkataba mpya,", alisema Koeman  juu ya Lukaku mwenye umri wa miaka 23 ambaye mkataba wake wa sasa utamalizika 2019.
Kauli hiyo ya Koeman inazidi kuzipa nguvu Manchester United na Chelsea ambayo zote zinawania saini ya Lukaku.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac